Naibu waziri Kienzile afungua mkutano wa 18 WA wadau sekta ya uchukuzi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 17 December 2025

Naibu waziri Kienzile afungua mkutano wa 18 WA wadau sekta ya uchukuzi

 



Na Queen Lema, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com


Serikali imesema itaendelea kuwekeza zaidi kwenye sekta ya usafiri Ili kuruhusu maendeleo kwenda kwa Kasi zaidi kwani sekta ya usafiri inachangia maendeleo ya jamii.


Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa uchukuzi, Davie kianzile kwenye ufunguzi wa mkutano wa 18 wa tathimini ya sekta ya uchukuzi


Kianzile alisema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa kwani sekta ya barabara na sekta ya Anga nayo kwa Sasa inafanya vyema Zaidi


"Serikali itaendelea kutimiza majukumu yake ipasavyo na itatimiza kwa kina Sana katika sekta za maji,barabara,na Anga  na mpaka sasa sekta zote hizo zimeshapiga hatua kubwa sana"aliongeza.


Alifafanua kuwa hata kwenye sekta ya usafiri wa Reli kwa mwaka jana idadi ya abiria ilikuwa ni chini ya milioni 2 lakini Kwa sasa abiria ni karibia zaidi ya milioni 8 wameweza kusafiri kwa kutumia Treni.


"Ndugu washiriki mnaweza kuona tofauti hiyo ilivyo kubwa na kiasi cha zaidi ya Bilioni 88,ambapo pia abiria walikuwa wanatokea Dodoma,Dar pamoja na Tabora"aliongeza


Katika sekta hiyo ya Reli alisema kuwa tayari wameshaini mkataba mpaka wa kwenda nje ya nchi,kuunganisha Sgr pamoja na nchi ya burundi ambapo wao wanaona ni mafanikio makubwa Sana.


Naye Katibu mkuu wizara ya uchukuzi Profesa Godius kaiyarara amesema kuwa sekta ya uchukuzi imesababisha kiwango kikubwa cha uchumi kukuwa kwa kiwango kikubwa 


Profesa huyo alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za B O t za mwezi uliopita sekta ya usafiri ilichagia Dola zaidi ya billion 2.6 jambo ambalo ni hatua kubwa sana.


Akiongelea alisema kuwa sekta ya usafiri inachangia zaidi ya asilimia 8 ya Ajira hapa nchini Jambo ambalo ni mafanikio makubwa Sana.


Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali Wa usafiri ambapo kwa pamoja wameweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo sekta ya usafiri.


Mwisho

No comments: