Na Queen Lema Arusha
maipacarusha@gmail.com
Taasisi za Dini zimeshauriwa kuhakikisha kuwa mbali na kuwalea vijana katika malezi ya kiimani wanatakiwa pia kuhakikisha wanawafundisha vijana stadi mbalimbali za kazi za mikono Jambo ambalo litaweza kuwasaidia kwenye maisha Yao ya baadae
Kwa sasa ni vema kama jamii ikahakikisha kuwa kila mtoto anafanya stadi mbalimbali za kazi Ili Hapo baadae waweze kufikiria hata namna bora ya kujiajiri
Hayo yameelezwa Jumapili iliopita na Bw James Mollel ambaye ni Muinjilisti Wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Olkeryan Morombo Jijini Arusha wakati akiongea na wazazi,walezi,waumini WA kanisa Hilo kwenye ibada rasmi ya kuwapokea vijana waliohitimu mafunzo ya kipaimara
James alidai kuwa katika nyakati za sasa asilimia kubwa ya vijana wanashindwa kuwajibika ipasavyo katika kazi mbalimbali za kijamii tofauti na Miaka iliopita Kitu ambacho sasa jamii inatakiwa kushituka Kwa haraka.
Aliendelea Kwa kusema kuwa stadi za kazi mbali na kuwaimarisha vijana lakini pia stadi za kazi zinaweza kuwa kichocheo kikubwa sana kwa vijana hao kuanza kufikiria namna ya kujiajiri na hivyo Taifa kuondokana na ukosefu Wa Ajira.
"Unajua Kwa sasa wapo vijana Ambao wanazunguka na bahasha kila maali wakiwa wanatafuta ajira lakini kumbe wakati wakiwa wanasubiri Ajira wangeweza kufanya hata vishuguli vidogo vidogo ambavyo vingewaingizia vipato,sasa sisi kama kanisa,sisi kama wadau wa Jamii tumeliona Hilo na tumeanza kuhakikisha kuwa wanafanya stadi za kazi Kwa ajili ya maandalizi ya Hapo baadae"aliongeza
Katika hatua nyingine Alisema kuwa nao wazazi Wa sasa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaachana na ile dhana ya kuwabembeleza watoto na kuona kama wakifanya kazi wanaonewa au wanateswa na badala Yake wahakilishe kuwa kila kijana au mtoto anajifunza mambo mbalimbali ya stadi za mikono.
"Kuwafundisha watoto kazi sio kuwatesa Bali ni kuwaanda Kwa ajili ya maisha ya Hapo baadae na kazi ni mpango halisi Ambao unaanzia kuanzia kwenye fikra hivyo basi kila mzazi sasa aache kuwabembeleza watoto na kisha kuwaambia wasifanye kazi"aliongeza
Kwa upande wa vijana waliotimu Kwa siku hiyo walisema kuwa pamoja na kwamba kanisa Hilo la KKKT olkeryan limeweza kuwafundisha masomo mazuri na stadi za kazi bado wazazi Wana nafasi kubwa ya kuhakikisha hata watoto kuanzia umri wa kuzaliwa wanalelewa katika misingi thabiti ya Kiimani na hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa sana Jamii kutokuwa na matukio mengi ya kutisha.
Watoto hao waliwataka wazazi kuhakikisha kuwa mbali na kuwalea wanatakiwa pia kukuza vipaji vyao Kiimani lakini Kwa njia ya stadi za kazi Ili kuweza kuwaraisishia maisha yao ya Hapo baadae
Jumla ya vijana132 kutoka katika kanisa hilo wameitimu mafunzo ya darasa la kipaimara lakini pia mafunzo ya stadi za kazi.
Mwisho

No comments:
Post a Comment