TANAPA YATWAA TUZO YA HUDUMA BORA YA KIMATAIFA (ESQR) 2025 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 14 December 2025

TANAPA YATWAA TUZO YA HUDUMA BORA YA KIMATAIFA (ESQR) 2025

 



Na mwandishi wetu


maipacarusha@gmail.com


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetunukiwa Tuzo ya Utoaji Huduma Bora ya Kimataifa kwa mwaka 2025 na European Society for Quality Research (ESQR) ya Uswisi, likiendelea rekodi yake ya ushindi kwa mwaka wa saba mfululizo tangu 2020. Tuzo hizo zilitolewa katika hafla iliyofanyika Dusit Thani Dubai, zikithibitisha ubora wa TANAPA katika sekta ya uhifadhi na utalii miongoni mwa taasisi 49 kutoka nchi 41 duniani.


Ushindi huo umetokana na kuzingatia kwao misingi ya maadili kama Utaalamu, Uwajibikaji, Uadilifu, Ubunifu na Ubora, sambamba na kanuni za usimamizi wa ubora za kimataifa (ISO). Misingi hii imeiwezesha TANAPA kutoa huduma zinazokidhi viwango vya kimataifa na kuimarisha nafasi yake kama taasisi inayoongoza katika uhifadhi na utalii duniani, pamoja na sekta nyingine nyingi zilizotambuliwa mwaka huu kama afya, elimu, ujenzi, teknolojia na madini.


Tuzo hii ni fahari kwa TANAPA na taifa kwa ujumla, Tunatoa wito kwa wa Tanzania kushiriki kwa asilimia kubwa kushiriki UTALII WA NDANI ili kujionea uzuri wa vivutio tulivyonavyo vinavyo tuletea heshima katika mataifa mengine. Hii inaonyesha dhamira ya Tanzania katika kuhifadhi na kutangaza urithi wa asili na kutoa huduma bora za uhifadhi na utalii endelevu. Hafla ya kupokea tuzo iliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Nkoba Mabula, akiwa na uongozi wa TANAPA akiwemo mjumbe wa Bodi ya Wadhamini TANAPA , CPA(T) Hadija Ramadhani , Kamishna wa Uhifadhi CPA Musa Nassoro Kuji  pamoja na watumishi wa TANAPA.

No comments: