Viongozi wa dini wakosa usingizi kuelekea Disemba 9 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 1 December 2025

Viongozi wa dini wakosa usingizi kuelekea Disemba 9





Burhani Yakub,Tanga.


maipacarusha20@gmail.com 


Viongozi wa dini wa Mkoa wa Tanga wametaja sababu kuu mbili zinazowakisesha usingizi kuelekea Disemba 9 kuwa ni kutokana na kuwa mpakani na nchi jirani na utulivu uliopo.


Wakizungumza wakati wa kikao cha amani cha viongozi wa dini wa Mkoa wa Tanga wamesema sababu hizo mbili zinahitaji kufanyiwa kazi ya ziada Ili Disemba 9 ipite kwa amani.


Sheikh Mohammed Dhikiri amesema Mkoa wa Tanga kuwepo katika mpaka na nchi jirani ni sababu tosha ya kuwasukuma wananchi pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kuacha kubweteka badala yake zichukuliwe tahadhari ya kila eneo.


Sababu hiyo imeelezwa pia na Sheikh wa Baraza kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Tanga,Sheikh Luwuchu ambaye amesema kutokana na kuwa mpakani ni wazi kuwa lazima tahadhari zichukuliwe Kwa kila mwananchi.


"Jukumu la ulinzi wa Mkoa wa Tanga si la viongozi wa Serikali au vyombo vya dola..ni la kila mwananchi na sisi viongozi wa dini tunapaswa kuongeza Dua na sala kila mara"amesema Sheikh Luwuchu ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya amani ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Tanga.


Mchungaji wa kanisa la Pentekosri Kange,Sayuni Kubeje amesema Kwa kawaida eneo ambalo Lina asili ya utulivu mara nyingi hulengwa na wenye nia ovu kuelekeza nguvu zao katika kufanya uhalifu.


"Tanga ni eneo pekee nchini ambalo hakukuwa na rabsha ya maandamano wakati wa uchaguzi...tusibweteke Kwa sababu waovu wanaweza kuelekeza nguvu zao katika kufanya uhalifu Ili kutekeleza malengo yao siku ya Disemba 9 2025.


Katibu wa jukwaa la viongozi wa dini Mkoa wa Tanga,, Mchungaji Daniel Msumari amesema lengo la kikao hicho ni kukusanya maoni ya viongozi wa dini kuhusu nini kifanyike kuepusha vurugu Disemba 9 pamoja na siku zijazo.


"Tutatembelea kila Wilaya za Mkoa wa Tanga kukusanya maoni ya viongozi wa dini kuhusu nini kifanyike kuepusha vurugu Disemba 9... Mwenyekiti wetu Sheikh Luwuchu amekuwa akisisitiza kuongeza dua na sala kwa kila nyumba ya ubada"amesema Mchungaji Msumari.


MWISHO

No comments: