Na Queen Lema,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Zaidi ya wananchi 200 kutoka katika makundi matano ndani ya Jiji la Arusha wamefanikiwa kupewa mafunzo na elimu sahihi kuhusu umuhimu Wa bima ya afya Kwa wote.
Akiongea Leo na makundi hayo mkuu Wa wilaya ya Arusha,Joseph Mkude alisema kuwa waliofanikiwa kupatiwa mafunzo hayo watakuwa mabalozi wazuri wa mpango huo wa Bima ya afya kwa watu wote
Mkude alisema kuwa mpango WA bima Kwa wote ni mpango Ambao ni sahihi na utaweza kuwasaidia wananchi wote kuanzia ngazi ya kaya
Alifafanua kuwa mpango huo unatakiwa uweze kwenda moja kwa moja Kwa wananchi kupitia wanufaika waliopata mafunzo Ili wananchi waweze kuujua Kwa kuwa Kwa mujibu Wa sheria unawataka wananchi wote waweze kunufaika na mpango huo
"Huu mpango Kwa ngazi ya Taifa umeanza lakini sisi Arusha ndio WA kwanza, kuuzindua na tunawaomba sana muwape elimu wananchi Ambao wakati mwingine wanateseka kutokana na kukosa fedha za kujitibu hasa wanapoumwa na wananchi wajue kabisa mpango huu wa bima kwa wote utaweza kuchangiwa kiasi cha Laki Moja na Nusu Pekee"aliongeza
Wakati huo huo aliwataka viongozi wa ngazi ya kata kuweka utaratibu maalumu wa kuhakikisha kuwa kila kaya inajua umuhimu WA Jambo Hilo lakini pia umuhimu wake
Naye Miraji Kisiwe Kutoka Nhif alisema kuwa mpango wa Bima kwa wote umewagusa watu makundi yote na wote wataweza kupata matibabu Kwa unafuu
Miraji alidai kuwa mpango huo umeletewa na Serikali ya sasa baada ya kuona kuwa upo umuhimu wa kuwa na uhakika wa matibabu kwa kuwa magonjwa huja bila taarifa
"Mfumo wa bima za afya kwa wote ni mzuri sana napenda kuwasisitizia wanufaika wa mafunzo haya muhakikishe kuwa mnaufikisha hata ngazi ya kijiji ili mfumo huu ufikie malengo yake"aliongeza



No comments:
Post a Comment