Na Queen Lema, Arusha
maipacarusha@gmail.com
Wadau pamoja na wataalamu wa mionzi nchini wameaswa kuhakikisha kuwa wanazingatia matumizi sahihi ya mionzi kwa mujibu wa Sheria Ili kuepusha jamii na matatizo mbalimbali hasa kwa matumizi yaliozidi
Kauli hiyo imetolewa na Bw Peter Pantaleo ambaye ni Kaimu Mkuu Ofisi ya Kanda ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania wakati akifunga rasmi mafunzo kwa wataalama wa Radiolojia zaidi ya 90 waliopatiwa mafunzo yaliyoandaliwa na TAEC
Pantaleo alifafanua kuwa wataalamu wa mionzi wanapotumia mionzi kwa kiwango kikubwa sio sahihi kabisa kwa afya zao hivyo basi ni muimu watumie mionzi kwa kiwango kidogo.
"Unakuta mgonjwa ameletwa kwenye miozi tupo na mwangalizi wake sasa kama mtaalamu hautakuwa makini unaweza kusababisha madhara makubwa na ndio maana nasisitiza matumizi yawe ni kadogo "aliongeza
Naye Mungubariki Nyaki ni mkufunzi wa mafunzo TAEC aliwasisitiza waajiri wote kwenye sekta hiyo kuhakikisha kuwa kila mara wanawapa ruhusawafanyakazi wao waweze kushiriki katika mafunzo mbalimbali ili wafanye kazi zao kwa umaskini mkubwa.
"Kila siku kuna teknolojia mpya zinazaliwa na teknolojia hizo kama hauna mafuzo sahihi huwezi kufanya kazi ipasavyo sasa kila mara waajiri wenu wahakikishe kuwa wanawapa fursa ya kushiriki mafunzo kama haya"aliongeza Nyaki.
Nao washiriki wa mafunzo hayo waliwataka waajiri kuachana na tabia ya kuona kuwa wanapowasaidia au kuwawezesha kwenda kushiriki kwenye mafunzo wanapoteza fedha zao mafunzo hayo ni muimu sana kwenye sekta ya afya
Mwisho


No comments:
Post a Comment