Mikopo ya Asilimia 10 ya Halmashauri yawavutia wajasiliamali Pangani. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 22 January 2026

Mikopo ya Asilimia 10 ya Halmashauri yawavutia wajasiliamali Pangani.

Katikati ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Profesa Riziki Shemdoe akikabidhi hundi Kwa wajasilamali wa Wilaya ya Pagani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Tanga

Katikati ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Profesa Riziki Shemdoe akikabidhi hundi Kwa wajasilamali wa Wilaya ya Pagani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Tanga

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Profesa Riziki Shemdoe akikagua bidhaa katika moja ya banda la maonesho Jijini Tanga alipokuwa akikabidhi hundi Kwa wajasilamali wa Mkoa wa Tanga

Picha zote na Burhani Yakub



Burhani Yakub,Pangani

maipacarusha20@gmail.com


Wajasiriamali wa Wilaya ya Pangani wamesema ongezeko la utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu limeanza kuwavutia na kuwapa nguvu ya kujikita katika shughuli za uzalishajimali na biashara ili waweze kukuza kipato cha familia zao.




Wamesema hayo walipozungumzia kuhusiana na mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu iliyotolewa juzi kwa Halmashauri za Mkoa wa Tanga na Waziri nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Profesa Riziki Shemdoe.

Walisema katika kipindi cha miaka miwili wameshuhudia jinsi Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ilivyoongeza kiwango cha mikopo na hivyo vikundi pamoja na idadi ya wanufaika kuwa kubwa tofauti na ilivyokuwa awali.

Bakari Juma mkazi wa Pangani Magharibi anayejishughulisha na uchomeleaji vyuma alisema yeye pamoja na wenzake wameanza kuonja matunda ya mkopo kutoka Halmashauri ya Pangani kwa sababu kupitia shughuli za kutengeneza mageti wameweza kununua viwanja vya kujenga nyumba pamoja na kumudu gharama za kuwalipia ada za shule watoto wao.

“Ongezeko la mikopo ambayo imekuwa ikitolewa na Halmashauri ya Pangani imetuvutia vijana wengi ambao tulikuwa hatuna shughuli za kufanya hivi sasa tumeanza kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiliamali na uzalishaji…tunaomba hali hii iendlee ili itusaidie kukuza uchumi katika ngazi za kaya zetu”alisema Mwajuma Hassani wa Bweni mjini Pangani.

Mkuu wa Idara ya Maedeleo ya Jamii Wilaya ya Pangani,Sekela Mwalukasa aliifahamisha Mwananchi kuwa katika robo ya mwaka wa fedha uliopita Halmashauri hiyo ilitoa mkopo wa sh 49.Milioni kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu lakini lakini hivi sasa mkopo umeongezeka hadi kufikia sh 80.milioni.

“Katika mkopo huo wa sh 80.milioni ulitolewa wiki hii,vikundi vya wanawake wamekopeshwa sh 32.milioni,vijana wakipta sh 43,milioni huku watu wenye ulemavu wakikopeshwa kiasi cha sh 5.milioni…tunatarajia wataweza kukuza uzalishaji mali pamoja na uzalishaji utaongezeka ikilinganishwa na awali”alisema Sekela.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Batilda Burian alisema katika robo ya mwaka ya mkopo uliotolewa kwa halmashauri za Korogwe Mji,Tanga Jiji,Korogwe Vijijini,Lushoto na Pangani jumla y ash 2.761.bilioni huku vikundi vya wanawake vikiwa 155,vijana 71 na watu wenye ulemavu vikiwa 19.

“Kupitia mkopo huu wa sh 2.761 bilioni tunatarajia jumla ya ajira 1715 zitatolewa,hii ina maana wengi watanufaika kwa kuwa na shughuli za kufanya na siyo kukaa maskani kupiga soga…maana yake hata uhalifu utapungua ama kumalizika kabisa”alisema Balozi Buriani.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Prifesa Riziki Shemdoe aliziagiza Halmashauri zote nchini kutoa zabuni kwa vikundi vya wanawake,vijana na wenye ulemavu kwenye shughuli ambazo zinaweza kuendeshwa na vikundi hivyo kwa ufanisi.

“Nimetembelea kikundi cha ufatuaji wa matofali cha vijana pale gofu jijini Tanga,wanafanya kazi kubwa mno ni vyema zabuni za ununuzi wa tofali za taasisi za Serikali na binafsi zitolewe kwa vijana wale kwa sababu uzalishaji wao ni mkubwa na wenye ufanisi wa kutosha…nitoe agizo kwa halishauri zote nchini zenye vikundi kama hivi kuvipa zabuni ili kuviendeleza”alisema Profesa Shemdoe.

Hata hivyo alisema anazo taariza za baadhi ya kata vikundi vyake havijawahi kupewa mikopo na akaahidi kufanya ziara za kushtukiza za kuvitembelea ili kujua kwanini vinatengwa.

“Nitaanza kufanya ziara za kushtukiza,nitajipangia mwenyewe ni kata ipi nakwenda nikikuta kuna kata zilizotengwa katika kupewa mikopo itabidi wakurugenzi wa Halmashauri hizo watoe maelezo kwanini wasitupishe ili nafasi zao zichukuliwe na wengine”alisema Shemdoe.

MWISHO


No comments: