![]() |
![]() |
Na mwandishi wetu, maipac
maipacarusha20@gmail.com
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, ameahidi kuiombea Tanzania amani na utulivu, baada ya vurugu za Oktoba 29, mwaka jana, huku akidokeza amewahi kuishi nchini katika mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Ruvuma na Arusha.
Ahadi hiyo ya Papa Leo, imetokana na ombi lililowasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo alipomtembelea Vatican, kuwasilisha ujumbe wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
![]() |
Balozi Kombo amekutana na Papa Leo XIV, leo Jumatano Januari 28, 2026 saa chache kabla ya Katekesi ya kiongozi huyo wa kiroho Vatican.
Katika hatua nyingine, Balozi Kombo na ujumbe wake ulikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu, Paul Gallagher, ambaye pamoja na mambo mengine amewasilisha wito rasmi kutoka kwenye Ukulu Mtakatifu kwa Tanzania kufungua ubalozi Vatican. Kwa sasa Tanzania inawakilishwa kutokea Ujerumani.




No comments:
Post a Comment