Taasisi za Serikali za kibiashara zatakiwa kutangaza fursa zilizopo - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 9 January 2026

Taasisi za Serikali za kibiashara zatakiwa kutangaza fursa zilizopo

 







Na Queen Lema, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com


Viongozi pamoja na wakurugenzi waliopo chini ya wizara ya viwanda na biashara wametakiwa kujiwekea utaratibu wa kuweka na kutoa taarifa sahihi juu ya fursa mbalimbali za biashara zilizopo ndani ya nchi na nje ya nchi 


Aidha kwa sasa kuna fursa nyingi ambazo zipo lakini kutokana na kukosekana kwa taarifa ambazo sio sahihi kumesababisha baadhi ya watanzania kushindwa kunufaika kabisa



Hayo yalielezwa jana Arusha na aliyekuwa Naibu Waziri Wa viwanda na Biashara Patrobas katambi wakati akifungua kikao kazi cha menejimenti wizara ya viwanda na Biashara na Taasisi zake 


Alisema kuwa zipo fursa nyingi ambazo zipo lakini kutokana na kukosa taarifa sahihi bado jamii haijaweza kunufaika nazo ila kwa sasa ni vema kila taasisi iliyopo chini ya wizara ihakikishe inatangaza na kuibua fursa ambazo zipo.


"Biashara ndio inayooongoza Nchi, ili tuseme tumepiga hatua kubwa lazima biashara zifanyike tena kwa wingi sasa mimi ninachosema tuhakikishe kila mtu anajua na kutambua fursa zilizopo hii itaongeza kasi ya uchumi wetu"aliongeza.


Wakati huo huo aliwataka viongozi hao wa taasisi za kibiashara kuhakikisha kuwa wanawashirikisha wawekezaji wadogo lakini hata wakubwa kwenye suala zima la mnyororo wa thamani kwa kuwa napo Hapo bado kuna changamoto kubwa sana.


" Mtanzania akishaamua kuwekeza mahali hata kama ni mdogo tayari Yule tunamuita Mwekezaji sasa ni vema ashirikishwe kila hatua na mimi nadhani kama tutafanya ivi itatusaidia kuwavutia walio wengi"aliongeza



Naye Dkt Hashil Abdallah, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara alisema kuwa kikao hicho kinalenga kujadili mambo mbalimbali kwenye viwanda lakini pia Biashara 


"Kila robo ya mwaka tunakutana na tunajadili na hii imetusaidia sana kuweza kutatua matatizo kwa pamoja ambayo yanakabili viwanda lakini Biashara"aliongeza


Mwisho

No comments: