Mwandishi wetu,maipac.
maipacarusha@gmail.com
Wakazi wa mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wenye changamoto mbalimbali za kiafya sasa wataanza kupata tiba bila kumeza midonge wala kuchomwa sindano.
Tiba hiyo kutoka nchini Uingereza inajulikana kama phototherapy itaanza kutolewa kuanzia Januari 17 na madaktari bingwa.
Akizungumza na Maipac media Tanzania, Mtendaji mkuu wa Taasisi ya afya ya Life Wave Tanzania, Dr Sam Magesa anasema tiba hiyo ambayo ni rafiki kwa afya ya binaadamu ni mkombozi kwa wagonjwa.
" Wagonjwa wengi hivi sasa changamoto zao zimechangiwa pia na matumizi ya dawa kupita kiasi na hivyo magonjwa yamekuwa sugu na wengine kupata magonjwa mapya"amesema.
Amesema technolojia ya tiba ya phototherapy ni suluhu ya magonjwa mengi ambayo yamekuwa yakiwapata watu.
Dr.Magesa anasema wagonjwa wa magonjwa ya mfumo wa uzazi, maumivu ya mwili,magonjwa ya wanaume,magonjwa matumbo, Moyo na Mengine mengi tiba itatolewa.
Anasema tiba hii ya kisasa inatolewa na dawa kutoka uingereza na Life Wave Tanzania pekee ndio wanatoa huduma hiyo.
Kwa upande wake Profesa Suleiman Mwenda akizungumzia tiba hiyo amewataka wakazi wa Arusha kufika ukumbi wa golden Rose hoteli kuanzia January 17 kupata tiba .
Profesa Mwenda amesema kwa mkoa wa Kilimanjaro Januari 17 asubuhi tiba itaanza kutolewa Boma ,wilaya ya Hai.
Anasema.pia dawa za magonjwa mbalimbali zitatolewa na kuuzwa na akawataka wakazi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kujitokeza.kupimwa na kupata tiba.
Kwa maelezo kamili ya upatikanaji wa tiba unaweza pia kupiga simu namba 0686873 440 pia kwa namba ya Dr. Sam Magesa 0788 155 668.
![]() |
Mwisho



No comments:
Post a Comment