![]() |
Na Julieth Mkireri, Maipac Ludewa
maipacarusha20@gmail.com
WANANCHI zaidi ya 450 wa vijiji vya Tarafa ya Masasi na Tarafa ya Mwambao wameanza kunufaika na mgao wa mbegu bora za ufuta kilo 225 zinazotolewa bure na Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, ikiwa ni mkakati wa kuwawezesha kiuchumi na kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa, Omary Mkangama, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Olivanus Thomas, amezindua zoezi la ugawaji wa kilo 225 za mbegu bora za ufuta .
Mkangama amesema Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri imeamua kugawa mbegu hizo kama mkakati wa kuwawezesha wananchi kuanzisha na kukuza mazao ya biashara, hususan zao la ufuta linaloendelea kuonyesha ma
Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo, Dr. Festo Mkomba, wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa mbegu hizo uliofanyika katika kijiji cha Kipangala, Kata ya Luilo.
Dr. Mkomba amesema mbegu hizo zina uwezo wa kupandwa katika heka 225 na zinatarajiwa kuongeza tija katika kilimo, uzalishaji pamoja na kuinua uchumi wa wananchi mmoja mmoja na Wilaya ya Ludewa kwa ujumla. Aidha, amewatoa hofu wananchi kuhusu soko la zao la ufuta kwa kusema kuwa soko lake ni kubwa na halmashauri itaendelea kuwa bega kwa bega na wakulima kuhakikisha upatikanaji wa soko kwa urahisi.
Kwa upande wake, Afisa Tarafa wa Tarafa ya Masasi, George Kapongo, amewataka wananchi kuacha kilimo cha mazoea na kujikita katika kilimo chenye tija na cha kibiashara, akibainisha kuwa bei ya ufuta kwa kilo mwezi Mei mwaka jana ilikuwa kati ya shilingi 2,900 hadi 3,000, hivyo ni fursa muhimu ya kujikwamua kiuchumi.
Naye Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Godfrey Lufome, amesema zao la ufuta ni miongoni mwa mazao ya kimkakati yanayochangia kupunguza umasikini na kuongeza pato la mwananchi, wilaya na taifa kwa ujumla. Ameongeza kuwa halmashauri itawezesha uanzishwaji wa vyama vya ushirika kwa ajili ya kuimarisha soko la zao hilo.
Wananchi walionufaika akiwemo Nelson Ngonyani, John Ngatunga, Ignas Njohoka na Annamaria Haule wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mbegu hizo, wakisema ufuta utawasaidia kuwa na zao la pili la biashara sambamba na korosho, hivyo kuongeza kipato chao.
Vijiji vilivyofikiwa na mgao huo ni Kipangala, Luilo, Lifua, Lihagule, Kiyogo, Lihugai, Kingole, Iwela, Nkomang’ombe na Nsele.
Mwisho


No comments:
Post a Comment