Halmashauri ya wilaya ya Arusha imependekeza bajeti ya bilioni 75.4 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 22 February 2026

Halmashauri ya wilaya ya Arusha imependekeza bajeti ya bilioni 75.4

 


Na Queen Lema, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com 


Halmashauri ya wilaya ya Arusha imefanya mapendekezo ya bajeti ya kiasi cha Bilioni 75.4 kwa mwaka ujao ambapo katika bajeti hiyo kuna Neema kubwa Kwa wanafunzi wapya zaidi ya elfu 20


Aidha bajeti hiyo imegawanyika katika makundi ambapo pia imelenga kutatua changamoto mbalimbali za kijamii


Akiongea kwenye kikao cha Baraza la madiwani Juzi mwenyekiti wa halmashauri hiyo Baraka Simon alisema kuwa bajeti hiyo IPO katika sehemu mbili 


"Bilioni 75. 4 ni Kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini kwa upande WA mapato ya ndani ni Bilioni 9.2 tuna imani kubwa sana na hii bajeti na tunajua kuwa italeta mfanikio makubwa Sana na ni rafiki mkubwa sana "aliongeza 


Katika hatua nyingine Alisema kuwa bajeti hiyo imelenga pia kuandaa vyumba zaidi ya 200 Kwa ajili ya wanafunzi wapya  Wa kidato cha kwanza mwakani 


"Mwakani kutakuwa na mabadiliko ya mfumo wa elimu wanafunzi wa darasa la sita wakimaliza watajiunga na kidato cha kwanza lakini hata hao wengine nao wanatakiwa nao kuingia kidato cha kwanza tumejipanga vyema"aliongeza


Katika hatua diwani wa kata ya mlangarini Emanuel Mrema alia kuwa Wana shukuri bajeti hiyo kwa kuwa imeweza kugusa nyanja zote zinazoitajika 


Mrema Alisema kuwa pamoja na kuwa kuna changamoto kwenye baadhi ya kata lakini kupitia bajeti hiyo vijiji vyote vitanufaika 


Mwisho

No comments: