VYAMA VYA SIASA,MIGOGORO IPUNGUE ILI WANAWAKE,VIJANA NA WENYE ULEMAVU WAPATE NAFASI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 12 February 2026

VYAMA VYA SIASA,MIGOGORO IPUNGUE ILI WANAWAKE,VIJANA NA WENYE ULEMAVU WAPATE NAFASI

 

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Juma Ali Khatibu,






Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


VYAMA vya siasa nchini vimehimizwa kuimarisha mshikamano na kupunguza migogoro ya ndani ili kuimarisha demokrasia na ushirikishwaji wa makundi yote, hususan wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu.


Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Juma Ali Khatibu, amezungumza hayo mjini Morogoro wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya siasa,.


Khatibu alisema baraza lake linalenga kuona migogoro inapungua au kumalizika kabisa, huku nafasi za uongozi zikigawanywa kwa haki.


Alisema vyama vina wajibu wa kuhoji, kushauri na kushiriki kikamilifu katika kujenga Taifa kupitia ushauri kwa Serikali.


Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, nae akahimiza viongozi kuhakikisha wanazingatia masuala ya kijinsia ili kuwapa wanawake nafasi ya kushiriki siasa.


Alisema demokrasia ya kweli lazima iwe shirikishi kwa kuhakikisha wanawake na wanaume wanashiriki kwa uwiano sawa.


Mafunzo hayo yalihusisha majadiliano kuhusu marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, gharama za uchaguzi, sera za jinsia na kanuni za mwaka 2025.


Katibu wa United Demovratic Party UDP,  Swaum Rashid, alisema mafunzo hayo yataisaidia nchi kudumisha amani na utulivu.


Mwisho.

No comments: