WIZARA YA ELIMU YAITAKA TEWW KUSIMAMIA NIDHAMU, UWAJIBIKAJI NA UWEZI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 19 February 2026

WIZARA YA ELIMU YAITAKA TEWW KUSIMAMIA NIDHAMU, UWAJIBIKAJI NA UWEZI

 



Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com 


WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeitaka taasisi ya Elimu ya watu wazima(TEWW) kuendelea kusimamia nidhamu, uwajibikaji na uwazi wa utendaji wa taasisi hiyo kwani ni chombo muhimu katika kuendeleza elimu endelevu nchini.


Mkurugenzi wa elimu msingi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Abdul Mauld alieleza hayo mjini Morogoro akimwakilisha naibu katibu wa Wizara hiyo, wakati wa mkutano wa 16 wa Baraza la Wafanyakazi wa taasisi ya Elimu ya watu wazima(TEWW).


Mauld alisema pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali katika taasisi hiyo, wanapaswa kuendelea kushirikiana  na kuwa kiweledi ili kukabiliana nazo  huku wakifanya

changamoto ziwe fursa ya kuendeleza ubunifu zaidi katika kuzitatuta na hasa changamoto za kifedha. 


"Ushauri wangu kwenu ni kuendelea kuongeza wigo wa utolewaji wa 

programu na kutafuta vyanzo mbadala vya mapato kwa 

kuandika maandiko yatakayoleta miradi mipya, ambayo itawasaidia kuongeza mapato ya ndani na hatimaye kusaidia kutatua changamoto zilizopo,"alisema.


Mkurugenzi huyo pia alizungumzia miradi ya Integrated Programme for Out School Adolescents IPOSA-(Mpango wa elimu chengamani kwa vijana walio nje ya shule) na SEQUIP-AEP ambapo alisema TEWW chini ya Wizara yanelimu kwa kushirikiana na 

Ofisis ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, inatekeleza ujenzi katika Halmashauri 30 zinazotekeleza programu ya IPOSA katika mikoa sita ya Tanzania Bara

(Manyara, Shinyanga, Simiyu, Singida, Pwani na Tanga).


Aidha jumla ya karakana 27 zimekamilisha ujenzi ambazo zitaendelea kuwasaidia vijana walio nje ya mfumo rasmi wa kupata ujuzi wa mafunzo ya ufundi, Stadi za Maisha, Ujasiriamali na Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), ambapo kiasi cha sh bilioni 1,551,998,000 kimetumika kukamilisha ujenzi huo.


Katika mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari kwa njia mbadala nchini (SEQUIP-AEP) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2022 hadi 2025, jumla ya wasichana 13,272 waliokatiza masomo ya sekondari wamesajiliwa na kuendelea na masomo katika vituo 191 vinavyosimamiwa na TEWW na kwa mwaka 2025 jumla ya wavulana 1.731 pia wemesajiliwa ambao ni sawa asilimia 111 ikilinganishwa na lengo la kusajili wasichana 12,000.


"Wajibu wa baraza hilo ni kuhakikisha mnasimamia kwa umakini utekelezaji wa kazi 

mbalimbali ikiwemo miradi yote inayotekelezwa na TEWW, hususan miradi mikubwa ya kimkakati kama SEQUIP-AEP na IPOSA, ili matokeo yake yaendelee kuwanufaisha wananchi kwa kiwango kikubwa,"alisema mkurugenzi Mauld.


Akizungumzia katika mkutano huo, mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa TEWW ambaye ni mkuu wa taasisi hiyo Prof Philipo Sanga alisema kuwa kupitia mradi wa TEWW imefanikiwa kutekeleza ujenzi wa madarasa 

na majengo ya utawala katika mikoa 14 na kufanya ukarabati wa majengo ya TEWW katika 

mikoa 8 jambo linalodhihirisha matumizi yenye tija ya fedha za 

serikali.


Aidha TEWW kwa kutambua umuhimu na kukidhi matakwa ya kisheria ya kuwepo Baraza la wafanyakazi katika sehemu za kazi, imekuwa ikifanya vikao vyake vya Baraza.


Mwisho.

No comments: