CCM SIMANJIRO WAENDELEA NA ZIARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 20 March 2026

CCM SIMANJIRO WAENDELEA NA ZIARA

 


Na Mwandishi wetu, Simanjiro 


SEKTRETARIETI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imeendeleza na ziara ya kata mbalimbali ili kushukuru, kusikiliza kero na kukagua uhai.


Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Wambura Igembya ameongoza wajumbe wa sekretarieti hiyo katika ziara ya kutembelea kata hizo.


Wambura ameongozana na wajumbe wa sekretarieti ya CCM ya Wilaya hiyo, akiwemo Katibu Mwenezi Mosses Makeseni, Katibu wa Wazazi Sasi Mirumbe na Katibu wa UWT Tichomo Sangija


Amesema lengo la ziara hiyo ni kuwashukuru wana Simanjiro kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2026, kusikiliza kero zao na kukagua uhai wa chama.


"Tunawashukuru wana Simanjiro kwa kumpa kura nyingi za kishindo Rais Samia Suluhu Hassan, kumchagua mbunge kwa tiketi ya CCM James Ole Millya ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuwachagua madiwani wa CCM," amesema Wambura.


Amesema katika ziara hiyo wataanza kwa kuzitembelea kata mbalimbali ikiwemo Loiborsiret, Naberera, Orkesumet, Ruvu Remit na Msitu wa Tembo.


Mwenyekiti wa kijiji cha Namalulu, Marumai Kirikai amemshukuru Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo na sekretarieti yake kwa ziara hiyo ambayo imewapa faraja na kuwaunganisha upya.


"Pamoja na ziara hii nzuri pia imetibu majeraha kwa baadhi ya viongozi waliokuwa na kambi tofauti, kumaliza tofauti na kisha wakakumbatiana na kushikana mikono kuashiria mwanzo mpya mzuri," amesema Marumai.


Diwani wa kata ya Ruvu Remit Yohana Maitei Kadogoo amesema wanampongeza Katibu wa CCM wa wilaya hiyo na sekretarieti yake kwa kufika katika kata yake na kuzungumza nao.


"Kwa namna moja au nyingine wana CCM wa Ruvu Remit wamepata na kupokea nasaha nzuri na maelekezo ya chama hivyo tunaahidi kutekeleza yote.


MWISHO

No comments: