Dkt Samia: Ngorongoro ni almasi yetu, mali yetu na urithi wa Dunia - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 12 March 2026

Dkt Samia: Ngorongoro ni almasi yetu, mali yetu na urithi wa Dunia

 







 Na mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com 


Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni kama almasi ya Tanzania na urithi wa dunia, hivyo Serikali haina budi kulienzi kwa kuwa ni tunu iliyoletwa nchini na Mungu.


Dkt Samia ametoa kauli hiyo, leo Alhamisi Machi 12, 2026, wakati wa hotuba yake, katika hafla ya kupokea taarifa ya Tume za Rais kuhusu mgogoro wa ardhi na uhamaji wa hiari, Ngorongoro.


“Wale wote wanaoleta maneno kwa faida zao kwa wanayoyaona wao, sisi Ngorongoro Mungu ameishusha kwetu, kwa hiyo ni yetu na pia ni urithi wa dunia. Hatuna budi kuienzi tunu hii ambayo Mungu ametujaalia,” amesema.


Amesema ni wajibu wa Serikali kuyalinda na kuyahifadhi maeneo hayo kwa mustakabali wa maslahi ya wenyeji wa eneo husika, Taifa na Dunia kwa ujumla.

No comments: