KUELEKEA UZINDUZI WA WAZOHURU APARTMENTS VIFAA VYA MICHEZO VYA MIL 4 VYATOLEWA KWENYE SHULE ZA MSINGI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 26 March 2026

KUELEKEA UZINDUZI WA WAZOHURU APARTMENTS VIFAA VYA MICHEZO VYA MIL 4 VYATOLEWA KWENYE SHULE ZA MSINGI

 


Mdau wa Maendeleo Mathias Canal achangia shule za msingi Manispaa ya Singida


Na Lilian Kasenene.



Maipacarusha20@gmail.com


KAMPUNI ya Wazohuru Media Group Limited amechangia vifaa vya michezo vya thamani ya shilingi milioni 4.2 kwenye shule za msingi katika Manispaa ya Singidaikiwa ni kuelekea uzinduzi wa WazoHuru Air BnB Apartments.


Vifaa hivyo vya michezo ni pamoja na jezi Jozi moja yenye jezi 16 na mpira mmoja katika shule ya Msingi Tumaini Viziwi, shule ya msingi Ukombozi, shule ya Kindai, shule ya msingi Sumaye, shule ya msingi Mtipa na shule ya msingi Unyankae.


Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Ltd Mathias Canal alisema kuwa Lengo kuu la zoezi ni kuhamasisha michezo mashuleni, kukuza vipaji vya wanafunzi, pamoja na kuchangia maendeleo ya afya na ustawi wa watoto.


Canal alieleza kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia kampuni yake imekabidhi vifaa hivyo vya michezo ikiwa ni sehemu ya mrejesho katika jamii baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo 7 ya WazoHuru Apartments yaliyopo Mtaa wa Unyankae - Miembeni Manispaa na Mkoa wa Singida


Mathias alibainisha kuwa March 28 Machi 2026, mradi huo wa eneo la makazi ya kisasa utazinduliwa ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo atakuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego.


Pia alichangia Jozi moja yenye jezi 16 na mpira mmoja kwa timu ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) Manispaa ya Singida kwa ajili ya kuanza mashindano ya michezo hiyo mwaka huu 2026.


Mwisho.

No comments: