![]() |
| Walter John Mbaga mhariri wa kituo cha Radio Lumen Karatu |
![]() |
| Nobert Hongoli mtangazaji wa Lumen Radio karatu |
Mwandishi wetu,Karatu
maipacarusha20@gmail.com
Watangazaji Wawili wa kituo cha Lumeni Radio cha Karatu, Mkoa Arusha, Nobert Hongoli na Wolter John Mbaga (Mhariri) wamekamatwa na kuwekwa rumande Kwa amri ya Mkuu wilaya hiyo Lameck Karanga.
Watangazaji hao wamekamatwa leo March 27, 2026 asubuhi baada ya agizo la Mkuu wa wa Wilaya ya kuwataka wafike Ofisini kwake na Baadae kuamuru kukamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Karatu
Mkuu huyo wa wilaya anawatuhumu watangazaji hao Kwa kosa la kuandika na kutangaza Habari za kuleta taharuki kwenye jamii habari yenyewe inahusu wananchi kuhofia mafuriko baada ya Bwawa kujaa hivyo wanaomba Serikali kuchukuwa hatua.
Kamanda WA polisi Mkoa Arusha , Justine Masejo alisema Hana taarifa za kukamatwa waandishi Hao na aliahidi kufatilia.
"Sina hizi taarifa ntazifatilia lakini pia mtafuteni na Mkuu wa wilaya kuhusu Jambo hili"alisema
Akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) Mussa Juma , Mkuu huyo wa wilaya aliahidi waandishi hao wataachiwa Leo.
Mwisho



No comments:
Post a Comment