DC MWEMA AKABIDHIWA RASMI NA RC SENDIGA JENGO LA OFISI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 30 April 2026

DC MWEMA AKABIDHIWA RASMI NA RC SENDIGA JENGO LA OFISI

 



Na Mwandishi wetu, Kiteto 


MKUU wa Wilaya ya Kiteto  Mkoani Manyara, Remidius Mwema, amekabidhiwa rasmi jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto na Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga, lenye thamani ya Shilingi bilioni 1.7 lililopo Mtaa wa Msakasaka, Kata ya Bwagamoyo, Tarafa ya Kibaya Wilayani Kiteto.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sendiga amekabidhi jengo hilo baada ya kukagua na kujiridhisha na hatua ya ukamilishaji wa mradi huo wenye vyumba 35 na ukumbi wa mikutano ambao umetekelezwa kwa mfumo wa force akaunti tangu  kuanza kwake  tarehe 30 Machi, 2023.


“Nawapongeza wataalamu na mafundi wote walioshiriki kufanikisha ujenzi huu, uzuri wa jengo hili ni lazima uende sambamba  na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kutoa tafsiri halisi ya uwajibikaji na utendaji kazi na huduma kwa wananchi” amesema Sendiga.


Hata hivyo, DC Mwema ameishukuru Serikali kwa kufanikisha mradi huo mkubwa na kuahidi kutekeleza kikamilifu maelekezo yote ya RC Sendiga kuhusu mradi pamoja na kuendelea kuifanya ofisi hiyo kuwa kimbilio la kila mwananchi wilayani Kiteto.


"Ni kweli jengo  linapendeza sana kwa muonekano wake, ahadi yetu ni kuongeza furaha mioyoni mwa wananchi kwa usikivu  na huduma kwa makundi yote ya wananchi, bahati nzuri miundombinu ya ofisi hizi inawezesha na watu wote wenye mahitaji maalum kuhudumiwa,” DC Mwema.


Mwenyekiti wa kitongoji cha Msakasaka kata ya Bwagamoyo  Mwangao Sadick Mpalila amesema mradi huo umesogeza karibu huduma kwa wananchi na kwamba  uwepo wa jengo la utawala la Wilaya katika mtaa huo pia itasaidia wananchi wengi zaidi  sasa kupata huduma kwa haraka na wakati mmoja.


MWISHO

No comments: