Dkt Samia: Napunguza msafara wangu kupunguza matumizi ya mafuta - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 8 April 2026

Dkt Samia: Napunguza msafara wangu kupunguza matumizi ya mafuta

 


Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametangaza mpango wa kupunguza ukubwa wa msafara wake, ikiwa ni hatua za mwanzo za kukabili matumizi ya mafuta, kutokana na kupanda kwa bei ya nishati hiyo duniani.


Katika utekelezaji wa hilo, Dkt Samia amesema wakuu mbalimbali wa idara wanaoongozana naye katika misafara hiyo wakiwa na magari yao, kwa sasa wote watapanda kwenye basi moja na kuacha magari yao.


Dkt Samia ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dodoma leo, Jumatano Aprili 8, 2026, alipohutubia baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua wiki iliyopita.


“Msafara utakuwa gari yangu, escort yangu ya polisi na gari ya akiba nyuma, waliobakia wote nawaingiza kwenye basi tupunguze matumizi ya mafuta,” amesema.

No comments: