Mjumbe wa Tume ya Uchunguzi wa ghasia wakati na baada ya uchaguzi, Profesa Ibrahim Juma, amesema Tanzania kumezuka tabia hatari ya watu kuzima maoni ya wengine, huku wakitaka ya kwao pekee ndio yasikilizwe.
Tabia hiyo, amesema imedhihirika hata baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya tume hiyo, baadhi ya wajumbe wamepokea jumbe zaidi ya 300 za matusi katika simu zao, kutoka kwa watu hao ili kuzima maoni yaliyowasilishwa kupitia ripoti.
Profesa Juma, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, Jumanne Aprili 28, 2026 alipozungumza na wahariri na waandishi wa habari
"Baada ya taarifa kutoka tumepokea matusi zaidi ya 300 kwa sababu kuna mtu hataki maoni yetu yaliyopatikana kwa njia ya methodolojia ya kusikiliza watu yasiwafikie watu," amesema.
No comments:
Post a Comment