MWENGE WA UHURU KUPITIA MIRADI YA BILION 263 MKOANI PWANI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 18 April 2026

MWENGE WA UHURU KUPITIA MIRADI YA BILION 263 MKOANI PWANI

 




Na Julieth Mkireri,MAIPAC BAGAMOYO


maipacarusha20@gmail.com 


MWENGE wa Uhuru umepokelewa mkoani wa Pwani April 18 huku ukitarajiwa kukimbizwa katika miradi ya maendeleo 68 yenye thamani ya zaidi ya sh. 263 Bilion.


Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Albert Chalamila katika eneo la Mapinga Wilaya ya Bagamoyo Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema utakimbizwa katika Wilaya saba na Halmashauri tisa za mkoa huo.


Kunenge amesema kati ya miradi 68 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 23 itawekwa mawe ya msingi,21 itazinduliwa na 24 itakaguliwa.


Mkuu huyo wa mkoa amesema miradi hiyo imechangiwa na Serikali kuu sh.16.2 bilioni, Halmashauri za Wilaya sh. 1.62 bilioni pia  wananchi na wawekezaji wamechangia kiasi cha shilingi 180.7 Billion, wadau wa Maendeleo sh. 64.3 Billion  na michango ya Mwenge milioni 38.8.


Awali akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Albert Chalamila katika mkoa huo ulipokelewa April 13 ma kwamba umepitia miradi 35 yenye thamani ya sh 113.3 Billion.


Naye kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Wazo Mwang'onda amesema kwakua Mwenge huo ni wananchi unatakiwa kukimbizwa kwenye maeneo ya wananchi


mwisho.

No comments: