![]() |
| Programu meneja wa TLS Kefar Mbogela akizungumza na waandishi wa habari |
Na Mwandishi wetu ,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Chama cha wanasheria Tanganyiika (TLS) kimefanikiwa kutoa elimu kwa wanasheria zaidi ya 500 kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenye juma la mawakili ambalo linaendelea jijini Arusha
Akizungumza na waandishi wa habari, Programu Meneja kutoka TLS, Kefar Mbogela alisema kuwa ellimu hiyo imeweza kuwafikia wataalamu hao wa sheria kwa njiia ya mikutano kuanzia siku ya jumatatu mpaka sasa
Mbogela alisema kuwa wameweza kupata elimu mbalimbali ambapo elimu hizo zinalenga kuwafanya waweze kuwa imara zaidi kwenye kazi zao na lengo halisi ni waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana
Alifafanua kuwa kwa sasa hata kama ukiwa ni mwanasheria lazima kuna elimu ambazo zinatakiwa uwe nazo na endapo kama hautaomgeza au kutamani kujifunza ni wazi kuwa dunia itakuacha nyuma
"dunia ya sasa imebadilika kwa kiwango kikubwa sana , mfano mwanasheria asipojua elimu ya uwekezaji , au elimu ya afya ya akili ni wazi kuwa atakuwa kwenye wakati mgumu sana wa utekelezaji kwenye majukumu yake sasa sisi tumeamua kuwapa elimu wataalamu hawa wa sherika kwa kuhakikisha wanajiongezea utaalamu zaidi"aliongeza.
katika hatua nyingine alisema katika semina hizo pia makundi mengine ndani ya jamii wameweza kujumuika nao kwa kupata elimu ambapo elimu hiyo itaweza kuwasaida kwenye mambo yahusuyo Sheria
"tumeamua kuwaweka watu wengine ili wanapoitaji msada wa kisheria waweze kuja na kujumuika nasi hasa kwa jkuma hili ambalo tupo hapa Arusha na pia kuwajengea uwezo kuwa wanapokuwa na uitaji wanaweza kututumia sisi katika kutatua matatizo yao"aliongeza
ELIMU ambazio zimetolewa ni pamoja na elimu ya afya ya akili,uwekezaji, Taaluma,pamoja na ,maadili kwenye kazi,na ubobevu wa kisheria.
Nao washiriki katika Semina hizo walisema kuwa wamefanikiwa kupata maarifa mbalimbali ambayo yatawasaidia kwenye sekta nzima ya uwajibikaji huku wakiwashukuru TLS kwa kuwapa fursa hiyo.
MWISHO


No comments:
Post a Comment