
Wakili Dkt. Anna Henga mkurugenzi wa kituo cha kisheria na haki za binadamu (LHRC
![]() |
Na Queen Lema,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Imeelezwa kuwa ili wana habari waweze kuwa wabunifu kwenye kazi zao wanatakiwa kupewa uhuru mzuri wa kufanya kazi zao
Ukosefu wa uhuru kwa vyombo vya habari hapa nchini umesababisha baadhi ya waandishi kukosa uhuru wa kufanya kazi zao
Hayo yameelezwa na Dkt. Anna Henga ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha kisheria na haki za binadamu (LHRC) wakati akiongea kwenye mjadala wa uhuru wa vyombo vya habar ambao unaendelea Jijini Arusha
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimeshindwa kufanya kazi zao kwa weledi kwa kuwa kuna vitisho ambavyo vinasababisha ubunifu kukosekana kitu ambacho kinasababisha walaji wa habari kukosa vitu muhimu kwenye habari
Alisema kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa inawapa uhuru wa kutosha kwa vyombo vya habari lakini pia wakubali kukosolewa lakini pia wanahabari wanapokosea pia wapewe nafasi ya kusikilizwa.
![]() |
"Pamoja na kwamba wana habari wameminywa serikali inapaswa kuwapa nafasi hata kama wamekosea ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwasikiliza na sisi tunaamini kuwa kama watafanya ivyo ubunifu utakuwa ni mkubwa sana"aliongeza
Nao waandishi wa habari walioshiriki katika mjadala wa siku ya maadhimisho ya uhuru wa vya habari walisema kuwa wakati mwingine muingiliano wa sera unasababisha washindwe kuwajibika vyema kwenye utendaji kazi wao
Mmoja wa waandishi hao Bertha Ismaili alisema kuwa wakati mwingine wanashindwa kufichua baadhi ya mambo kutokana na kuwepo kwa mazingira ambayo sio rafiki baina ya Serikali,wamiliki
Alihitimisha kwa kuomba kuwepo kwa uwazi mzuri lakini pia kuwezeshwa kwa kila namna kufanikisha maitaji yanayoitajika ili jamii iweze kupata chakula cha habari.
Mwisho




No comments:
Post a Comment