BODI YA WAKURUGENZI (TPDC) YATEMBELEA MRADI WA EYASI -WEMBERE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 25 May 2026

BODI YA WAKURUGENZI (TPDC) YATEMBELEA MRADI WA EYASI -WEMBERE

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC Balozi Ombeni Sefue akiwa katika Ziwa Eyasi wakati wa Ukaguzi wa MRADI WA Eyasi-Wembere







Na.Ashura Mohamed -Karatu


maipacarusha20@gmail.com 


Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) imesema kuwa inaridhishwa na uwezo mkubwa wa shirika katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya Mafuta,ambapo hapo Awali kwa baadhi ya kazi  zilikuwa zikifanywa na wakandarasi kutoka nje ya nchi ambapo sasa zinafanywa na  wazawa.


Mwenyekiti  wa bodi   ya Wakurugenzi wa (TPDC),Balozi Ombeni Sefue alisema kuwa kazi nyingi za kitaalamu sasa  zinafanywa na vijana waliopo hapa  nchini  kwa  ubora ambao unatakiwa ikiwa ni pamoja na  wakandarasi wazawa  ambao wameajiriwa na TPDC.


Balozi Sefue aliyasema hayo mara baada ya kutembelea Mradi wa Utafiti wa Mafuta na Gesi wa Eyasi -Wambere uliopo Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha ili kujionea hatua mbali mbali za utekelezaji wa Mradi huo kabla ya kumalizika kwa Awamu ya kwanza mnamo mwezi June,2026.


Balozi Sefue alisema kuwa mpaka sasa zaidi ya shilingi bilioni 47 zimeshatumika tangu mradi ulipoanza mwaka 2015 hadi sasa 2026 ,ambapo fedha hizo zimetoka ndani ya TPDC na wanafanya hivyo kwa kuwa na Imani kuwa watapata matokeo mazuri pindi Utafiti utakapokamilika.


"Sasa utafutaji wa Mafuta una hatua nyingi kwasababu ni gharama kubwa sana kuchimba visima vya mafuta kwahiyo hutakiwi kuanza kuchimba kabla ya kufanya  hatua ya kwanza ikakupa matumaini alafu unaenda hatua ya pili na ya tatu mpaka mwisho unachimba kisima cha majaribio ili kupata Matokeo chanya"Alisema Sefue


Aidha alisema kuwa eneo hilo la Ziwa Eyasi limekuwa na changamoto kubwa ikiwemo kujaa tope,ziwa kukauka hali ambayo inapelekea mkandarasi kushindwa kufanya kazi kwa wakati licha ya vifaa vya kisasa alivyonavyo .

 

Kwa Upande wake meneja wa Mradi kutoka Eyasi -Wembere  Sindi Maduhu alisema kuwa sasa wapo katika hatua za  kuchukua za mitetemo ambapo sasa wanatarajia kukamilisha awamu ya kwanza ikiwa ni pamoja ma kuendelea kuongeza kasi ya ukusanyaji wa  taarifa nyingine ili kuepuka kuliingiza taifa kupata hasara.


Alisema kuwa kazi hiyo inafanywa na mkandarasi mzawa wa kampuni ya  African Geophisical Service  (AGS ),ambapo  imekuwa na mafanikio makubwa kwasababu ya  kutumia waaalamu wazuri  na mitambo ya kisasa kulingana na eneo la Mradi,ili kukamilisha kwa wakati na kwenda katika hatua inayofuata.


Kitalu hicho kinapitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) ambao utawezesha kusafirisha mafuta yatakayopatikana pindi yatakapogunduliwa, hatua inayotarajiwa kuongeza kasi ya shughuli za utafiti katika eneo hilo.


Mwisho

No comments: