Na mwandishi wetu,Dodoma
maipacarusha20@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Dkt Johannes Lukumayi ameomba wizara ya Mali asili na utalii kuongeza kiwango Cha miradi mbalimbali katika vijiji na kata ambazo zimepakana na vivutio vya utalii, katika Jimbo lake.
Mbunge huyo akiwasilisha ombi Hilo juzi kwa Naibu waziri wa Mali asili na utalii Hamad Chande, mbunge huyo alisema kuwa Bado vijiji vilivyopakana na maeneo ya vivutio Kuna changamoto mbalimbali ikiwemo uwepo na miradi michache
Dkt Lukumayi alisema kuwa wananchi wanaozunguka katika vivutio vya utalii wanatakiwa kuwa namba Moja kunufaika na vivutio hivyo
Aliongeza kuwa vivutio hivyo kama vile hifadhi ya msitu wa Meru,pamoja na hifadhi ya Arusha
Alisema kuwa ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kuangalia namna ya kurudisha fadhila kwa wananchi wanaozunguka vijiji vya vivutio hivyo
Dkt Lukumayi aliainisha kata na vijiji vinavyopakana na hifadhi ya msitu wa Meru -Usa ni pamoja na kata ya Oldonyosambu,Kata ya Olmtonyi,kata ya Kimunyaki pamoja na Kiutu
" Tunaomba Wizara kwa kushirikiana na Serikali sasa waweze kutusaidia katika miradi mbalimbali pamoja na kutatua changamoto zilizopo kama sehemu ya faida kwa jamii kwa kuwa wananchi wanatakiwa Kuona umuimu wa vivutio hivyo"aliongeza.
Kwa upande wake Naibu waziri wa maliasili na utalii,Hamad chande alisema kuwa amelichukua jambo Hilo na atalifanyia kazi ombi Hilo la Mbunge huyo ambaye amewasilisha .
Mwisho

No comments:
Post a Comment