![]() |
Na Queen Lema,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Viongozi Waandamizi wa Hospitali ya PSRI New Delhi India wanatarajia kufanya Ziara Nchini Tanzania, hususan Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Mwezi Juni, 2026 pamoja na Kuonana na Viongozi katika Ngazi husika kuweka Mikakati ya Utekelezaji kwenye sekta ya afya
Aidha ujio wa viongozi hao kutoka nchini India utaweza kuzaa matunda katika hospitali ya wilaya ya Olturment
Pia ujio wa viongozi huo unatokana na ziara ya Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mh.Dkt. Johannes Lembulung Lukumay aliyefanya ziara hiyo Machi 3, 2026, Hospitali ya PSRI New Delhi, India, na kufanya Kikao na Uongozi wa Hospitali hiyo.
Kikao kiliazimia, kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI kusaidia Hospitali ya Wilaya ya Olturumet kutoa Dawa na Vifaa Tiba, kutoa Mafunzo kwa Watumishi, kufanya Tafiti za Magonjwa Yasioambukiza na kubadilishana Watumishi kati ya Hospitali hizo Mbili ili Kupata Uzoefu wa Taaluma, kuimarisha Huduma za PHC na kuendesha Kiliniki ya Mikoba

No comments:
Post a Comment