![]() |
| Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi akifunga kikao cha Baraza la Madiwani lililofanyika hivi karibuni. |
NA SEIF TAKAZA – IRAMBA
maipacarusha20@gmail.com
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kyengege, Innocent Msengi, ametoa wito kwa madiwani kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo watendaji wa Kata na Vijiji katika ukusanyaji wa mapato.
Ametoa wito huo hivi karibuni katika Mkutano wa Baraza la Madiwani, kikao cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, kilichofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, ambapo amesisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa mapato ya ndani kwaajili ya maendeleo ya Halmashauri.
"Mapato ya ndani ndiyo msingi wa maendeleo ya Halmashauri ni wajibu wetu kusimamia kikamilifu ukusanyaji wake" alisisitiza.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Mkuu wa idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Morton Msowoya amesema kuwa mikakati mbalimbali imewekwa ili kuendelea kupanua wigo wa ukusanyaji mapato.
Kikao hicho cha Baraza la Madiwani kinachofanyika kila baada ya miezi mitatu, kimehudhuriwa na Madiwani wa kata zote 20, wakuu wa idara na vitengo, kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya pamoja na wananchi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleman Mwenda amehimiza uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma kwa wananchi.
Mwenda ameyasema hayo katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani, akisisitiza viongozi na watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa weledi. Akitoa maelekezo ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa watumishi wasio tekeleza wajibu wao ipasavyo.
Katika kikao hicho Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iramba Samwel Ashery ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ambayo imeelezwa katika kikao hicho. Hivyo anaomba watendaji na wataalamu wa halmasahuri hiyo kumuheshimisha Mbunge wetu Dr Mwigulu Nchemba Wilaya yetu iwe mfano wa kuigwa na wilaya zingine. Hata hivyo Mwenyekiti huyo alimpongeza Dr Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mbalimbali wa shughuli za kilimo, mifugo, miundombinu, ujezni wa madarasa, na shughuli za kijamii kwa ujumla.
MWISHO

No comments:
Post a Comment