Burhani Yakub, Tanga.
maipacarusha20@gmail.com
Serikali imeahidi kuwawekea mazingira mazuri mafundi wa fani mbalimbali Mkoani Tanga ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora wenye kuzingatia hadhi za kimataifa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dr Batilda Burian ametoa ahadi hiyo leo wakati akifungua kongamano la kuwajengea uwezo mafundi lililoambatana na uzinduzi wa Chama Cha Mafundi Tanzania ( CMT) Mkoa wa Tanga uliofanyika Jijini hapa.
Akizungumza kwa niaba yake ,Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Salum Nyamwese amesema kwa kutambua umuhimu na mchango mkubwa unaotolewa na mafundi katika kuendeleza uchumi wa nchi,Serikali imejipanga kuwawekea mazingira mazuri mafundi wa fani mbalimbali.
"Katika risala yenu mmeomba Halmashauri Wilaya zote za Mkoa wa Tanga zotenge maeneo maalumu ya gereji kuliko ilivyo sasa kila mmoja anafanyia popote...nimeshawasiliana Balozi Dr Batilda Burian ameahidi kulifanyia kazi haraka"amesema Nyamwese.
Mazingira mengine amesema kupitia mpango wa uboreshaji wa.mfuko wa bima ya afya kundi hilo litakuwa miongoni mwa wafaidika wa matibabu.
Mratibu wa mpango wa uboreshaji wa shughuli za Mafundi Mkoa wa Tanga,Said Mohamed amesema mafundi wa fani mbalimbali za ufundi nchini wameamua kuungana na kuunda chama kijulikanancho Chama Cha Mafundi (CMT) kitakachowasaidia kuwainua kiîchumi.
"Pamoja na kazi kubwa wanazofanya na mchango wao katika pato la Taifa lakini kuanzia mazingira ya ufanyaji kazi haviwanufaishi ...tumeamua kuungana ili kuwa na chombo ambacho kitaweza kuratibu shughuli zetu lakini pia kujuana nani yupo wapi na anafanya nini"amesema Said.
Mwenyekiti wa CMT Mkoa wa Tanga,Omar Mhando"Sir Omar"amesema miongoni mwa majukumu ya chama hicho ni kuwatafutia fursa maeneo mbalimbali za kazi mafundi kulingana na fani zao.
"CMT ni chombo ambacho kimekusanya mafundi wa fani zote lengo ni kutambuana na kisha kutafutiana fursa zitakazowawezesha kupata kazi na malipo yaliyo bora Omary"amesema Sir Omar.
Meneja wa benki ya NBC mkoa wa Tanga,Moses Mng'ong'o amesema lipo dirisha la mikopo kwa makundi na wafanyabiashara ambao kama watachangamkia watanufaika kiuchumi.
Meneja wa Shirika la Nyumba NHC Mkoa wa Tanga,Mussa amewataka mafundi wa fani mbalimbali kujitokeza kwa kuwa linaendesha ujenzi lakini wanaohitajika ni mafundi bora.
MWISHO

No comments:
Post a Comment