
Raisi wa TLS wakili Boniface Mwabukusi
Na Queen Lema Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Chama Cha wanasheria wa Afrika(PALU)kimesema Kuna umuimu wa Sheria kufuatwa na kuzingatiwa ipasavyo pamoja na kulinda Haki za binadamu hasa kwa nchi za Afrika.
Hayo yameelezwa na Ofisa mtendaji wa PALU, Donald Deya wakati akifungua mkutano mkuu wa chama Cha wanasheria Tanganyika (Tls) Arusha.
Alisema kuwa Haki za binadamu zinatakuwa kulindwa ipasavyo na kuheshimiwa hivyo jamii inapaswa kujua na kutambua kuwa Hilo linatakiwa kutekelezwa vyema.
" Ninyi vyama vya kisheria mnatakiwa kujua na kutambua kuwa mna wajibu wa kusimamia Sheria pamoja na haki ipasavyo msikubali Kuona haki za binadamu zikiwa zinavunjwa alafu mnakaa kimya kwa kweli ni mbaya sana
Na pia hata Tls nanyi pia muendelee kujitokeza kusimamia utawala wa Sheria kila maali mnapoona hapaendi sawa Hapo mtakuwa mmesaidia jamii yenu na bara letu kwa ujumla"aliongeza
Naye Raisi wa TLS wakili Boniface Mwabukusi alisema kuwa chama chake bado kipo kwenye mstari wa kuhakikisha kuwa Sheria inasimamiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutekeleza wajibu kwa mujibu wa taaluma
Mwabukusi alisema kuwa hawauzi wajibu wa kisheria Bali wanatekeleza na ni kwa maslai ya jamii
Wakati huo huo wakili Mwabukusi amelitaka Jeshi la polisi nchini kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanaokamatwa hawakaii nao sana Bali wafikishwe katika ngazi ya mahakama ili Hali iweze kutendeka.
Alihitimisha kwa kuwataka mawakili kusimamia ipasavyo maadili yao ya kazi pamoja na kutekeleza ipasavyo wajibu wao kwani kwa sasa TLS haitawafumbia macho wasio kuwa na maadili
Mwisho

No comments:
Post a Comment