Ofisi ya wakili mkuu wa serikali yaokoa zaidi ya Trilioni Moja - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 19 May 2026

Ofisi ya wakili mkuu wa serikali yaokoa zaidi ya Trilioni Moja

 



Na mwandishi wetu, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com 


Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa Sheria wameweza kuokoa kiasi Cha zaidi ya Trilioni Moja kutoka kwenye  mashauri  zaidi ya 565.


Hayo yameelzwa na wakili mkuu wa serikali,Dkt Ally Ponssi wakati akiongea na mawakili wa serikali kwenye ufunguzi wa semina uliofanyika Jijini Arusha


Dkt Ally alisema kuwa kiasi hicho Cha fedha kimeweza kuokolewa kutokana na ushirikiano  na mpaka sasa Ofisi yake inaendelea kuhakikisha inasaidia Serikali kuokoa fedha 


Alisema kuwa mawakili hasa wa Serikali wanaposimama na kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa inasaidia sana lakini wakili wa Serikali anaposhindwa kusimamia ipasavyo inasababisha serikali kujikuta ikiwa imeingia kwenye shida 


"Nataka niwaambie kuwa mawakili wa Serikali Tena chini ya Ofisi yangu wanafanya kazi kwa bidii sana na hii imeweza kuokolea Serikali hasara kubwa kutokana na Madai mbalimbali"aliongeza


Wakati huo huo aliwataka mawakili wa Serikali kuhakikisha kuwa wanatumia ipasavyo kalamu zao kuliko nguvu kubwa kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuruhusu Haki kuwepo pande zote mbili 


"Ninyi mawakili mnaweza kuhakikisha kuwa mnalinda amani ya nchi  kwa kumtumia kalamu zenu, na taaluma zenu,na mkizembea kidogo kwenye kazi zenu mtasababisha hasara nawasihi sana muhakikishe mnakuwa makini"aliongeza 


Wakati huo huo aliwataka baadhi ya mawakili kuhakikisha wanaacha tabia ya kutotoa taarifa kwa Ofisi ya wakili mkuu lakini kwa mwanasheria mkuu dhidi ya kesi yoyote ile hasa inayohusu Serikali


"Unakuta wakili anataarifa dhidi ya jambo luhusulo Taifa lakini ufuatiliaji unakuwa mdogo na hamna hata hiyo taarifa naomba sana kuanzia sasa tuhakikishe tunabadilika na tuwe wawazi kabisa juu ya kinachoendelea"aliongeza.

No comments: