![]() |
Rais wa Kenya, Dk William Ruto, amempongeza Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuonyesha uongozi kipindi cha kuzivuka changamoto zilizotokea Oktoba 29, mwaka jana.
Ruto, ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 4, 2026 baada ya kikao cha uwili na Dkt Samia Ikulu jijini Dar es Salaam. Ruto yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Katika maelezo yake, Ruto amemsifu Dkt Samia, akisema ameonyesha uongozi kwa kuunda tume ya kuchunguza mambo hayo na hilo limedhihirisha kuwa, mataifa ya Afrika Mashariki yanaweza kutatua changamoto zake ndani ya mipaka yake.
“Kwa niaba wa Afrika Mashariki, tunakupongeza kwa kuonyesha uongozi kwa Tanzania na ukanda wetu na kuhakikisha kwamba tunaweza kutatua matatizo yetu ndani ya mipaka yetu,” amesema.


No comments:
Post a Comment