Na Mwandishi wetu,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Toba Alnason Nguvila, amemuwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kufungua Kongamano la Wauguzi wa Afya nchini, linalofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha -AICC
Dkt. Nguvila, licha ya kuwapongeza wauguzi wote nchini kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutoa huduma bora za afya na kuokoa maisha ya wananchi kila siku amesisitiza nafasi kubwa waliyo nayo kwa maendeleo ya sekta ya afya nchini na jamii kwa ujumla wake.
Aidha, Dkt. Nguvila ameweka wazi kuwa moja ya vipaumbe vya Serikali ya awamu ya sita ni kuboresha huduma za Afya ikiwemo, uboreshaji wa miundombinu ya afya, uwepo wa dawa na vifaa tiba, jambo ambalo licha ya kurahisisha upataikanaji huduma bora za afya yanawarahisishia kazi Wauguzi katika kutoa huduma.
“Kuboresha huduma za afya ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan, sote tumejionea kazi kubwa imefanyika ya kuimarisha hospitali za Wilaya, Mikoa, Kanda na Hospitali ya Taifa na sambamba na uwepo wa Zahanatai kwenye vijiji na vituo vya Afya kwenye kata, lengo likiwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na bado kazi inaendelea"
Hali kadhalika vifaa tiba na uchunguzi vya kisasa vimeendelea kuwekwa na uwezo wa hospitali zetu kuchunguza na kutibu maradhi umekuwa mkubwa pamoja na kupanua fursa za mafunzo na ajira kwa Wauguzi na Wataalamu wengine wa afya.
Ameongeza kuwa, hata hivyo upande wa Serikali imejitahidi kuboresha kuendelea kuboresha maslahi ya wahudumu wa Afya kwa kadri Uchumi wa nchi utakavyokaa vizuri pamoja na kuendelea kutoa ajira mpya kwa wahudumu wa afya.
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani mwaka huu yamewakutanisha wadau wa sekta ya afya nchini kwa lengo la kujadili mafanikio, changamoto pamoja na njia bora za kuboresha huduma za afya kupitia kada ya uuguzi.
Awali, Mkutano huo ni mandalizi ya kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yanayofanyia Mei 12,2026, yaliyobeba Kaulimbiu ya “Wauguzi Wetu, Mustakabali Wetu; Wauguzi Waliowezeshwa Huokoa Maisha,”



No comments:
Post a Comment