SUA YAANZA UTAFITI KWA MIRADI 12 YENYE THAMANI YA SH. BIL. 3.4 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 22 May 2026

SUA YAANZA UTAFITI KWA MIRADI 12 YENYE THAMANI YA SH. BIL. 3.4

 









Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeanza utekelezaji wa miradi mipya 12 ya utafiti yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.4.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Raphael Chibunda


Hayo yamebainishwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Raphael Chibunda, wakati wa mahafali ya 47 ya chuo hicho, ambapo jumla ya wahitimu 877 walitunukiwa shahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba.


Alisema lengo la miradi hiyo ya utafiti ni kukuza maarifa na kutatua changamoto katika sekta za kilimo, mifugo, mazingira pamoja na maendeleo ya jamii kwa ujumla.


Profesa Chibunda alisema kuanza kwa miradi hiyo kumeifanya SUA kufikisha jumla ya miradi ya utafiti 130 inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.


“Chuo kinaendelea kuhimiza matumizi ya matokeo ya tafiti zetu katika kuchangia sera na mipango ya taifa. Katika kipindi hiki cha taarifa, chuo kimeanza utekelezaji wa miradi mipya yenye thamani ya shilingi bilioni 3.4,”alisema Profesa Chibunda.


Akizungumza katika mahafali hayo mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha SUA, Andrew Masawe, alisema Baraza limeendelea kutekeleza kwa kiasi kikubwa mambo yaliyolenga kuboresha sura ya chuo.


Masawe alisema chuo pia kinasimamia matumizi bora ya fedha na ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.


Alisema pamoja na mambo mengine, wameendelea kuhimiza ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya chuo kupitia mapato ya ndani, jambo ambalo limetekelezwa kwa ufanisi mkubwa huku miradi hiyo ikiendelea vizuri.


“Baraza limeendelea kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo kiasi cha shilingi bilioni 59.6 kimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” alisema Masawe.


wahitimu hao wamehitimu Shahada, Astashahada ya Umahiri na Shahada ya Uzamivu (PHD) ambazo wametakuwa kutambua kuwa kuhitimu katika Chuo Kikuu Sokoine haijawahi kuwa rahisi.


Mwisho.

 

No comments: