Wenger aisifu Serengeti Boys, asema Tanzania ina kizazi cha mabingwa wa soka - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 30 May 2026

Wenger aisifu Serengeti Boys, asema Tanzania ina kizazi cha mabingwa wa soka

 


Mkuu wa Maendeleo ya Soka wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Arsène Wenger, amesema mafanikio ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys, yanaonyesha kuwa Tanzania ina kizazi kipya cha wanasoka wenye uwezo wa kushindana na timu bora.


Kwa mujibu wa Wenger aliyewahi kuifundisha Klabu ya Soka ya Uingereza ya Arsenal, mchezo wa Tanzania dhidi ya Misri ulikuwa wa kiwango cha juu na ulionesha ubora mkubwa wa vijana hao.


Amewasifu kwa ujasiri, nidhamu ya kiufundi na mchezo wa kuvutia uliowafanya kuwa miongoni mwa timu zilizong'ara zaidi kwenye mashindano.


Serengeti Boys, imefuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia U17, inayotarajiwa kufanyika Qatar. Hata hivyo, mafanikio hayo ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji katika michezo.

No comments: