Marekani: CCM, wapinzani zungumzeni - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 18 June 2026

Marekani: CCM, wapinzani zungumzeni

 


Bunge la Seneti la Marekani limetaka kuanza kwa mazungumzo ya maridhiano kati ya Serikali inayoongozwa na CCM na vyama vya upinzani, ikiwa ni sehemu ya mapitio ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Tanzania.

Sharti hilo limejumuishwa katika Muswada wa Mapitio ya Uhusiano wa Uwili kati ya nchi hizo mbili, likisisitiza umuhimu wa viongozi wa kisiasa kukaa pamoja na kujadili mustakabali wa demokrasia nchini baada ya matukio yaliyoambatana na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025. 

Hatua hiyo inaonekana kuendana na msimamo wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye awali alieleza utayari wa kuanzisha mchakato wa maridhiano ya kitaifa na kutangaza mpango wa kuunda Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano wa Watanzania. Sharti hilo la Marekani, linaonyesha dhamira ya Taifa hilo kuendeleza ushirikiano na Tanzania.

No comments: