Na Mwandishi wetu, Meru
maipacarusha20@gmail.com
Imeelezwa kuwa ili walimu pamoja na wanafunzi kwenye halmashauri ya Meru waweze kufanya vyema kwenye mithiani ya kikanda, kimkoa, na kitaifa wanatakiwa kupewa motisha ikiwemo ya Mali zisizohamishika ili kuboresha zaidi elimu
Hayo yalielezwa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa halmashauri ya Meru, Bw Jeremiah Kishili alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi kwenye hafla ya ukabidhiwaji wa zawadi na tuzo kwa shule zilizofanya vyema kwenye mithiani ya Taifa.
Jeremiah alisema kuwa walimu wanapopewa motisha inawasaidia sana kuweza kufanya jitiada mbalimbali za kuwasaidia watoto wafanye vyema kwenye mithiani yao ya Mwisho
Alifafanua kuwa kwa sasa motisha kwa walimu unatakiwa uwe wa Mali ambazo haziamishiki ili mwalimu anapokabidhiwa iweze kuwa kama alama kwake
"Mwalimu anapopewa motisha ambayo haiamishiki hiyo ni ngao nzuri kwake lakini hata wenzake wanapoona inawasaidia sana kuweza kuongeza jitihada zaidi"aliongeza
Katika hatua nyingine Aliishukuru Halmashauri ya Meru kuweza kutoa usafiri kwa shule ya sekondari pamoja Ngabobo ambapo usafiri huo utaweza kuwasaidia vyema watoto
"Natoa wito lakini nashukuru Halmashauri kuweza kutoa gari kwa sekondari yetu, lakini nitumie nafasi hii katika kuhakikisha tunawasaidia watoto na shule mbalimbali za mji wa Meru nazo wanatakiwa kupatiwa usafiri naamini hii itasaidia sana"aliongeza
![]() |
Naye mmoja wa wadau wa elimu ambaye amechangia kwa kiwango kikubwa kwenye sekta ya elimu Meru, Bw Aminiely Kurie Nnko alisema sekta ya elimu inatakiwa kupewa kipaumbele sana lakini pia kutatua changamoto zilizopo kwenye baadhi ya shule
Kuriye alisema kuwa yeye akiwa kama mdau wa maendeleleo sekta ya elimu amechangia kwa kiwango kikubwa shule ya sekondari Seela na matokeo yalishaonekana
"Mimi ni mtanzania ambaye ni mzawa kabisa nimechangia sana kwenye sekta ya elimu, maendeleo ya kata,nawasihi na watanzania wengine wahakikishe kuwa wanaiga mfano huo"aliongeza
Mbali na hayo aliomba wadau wa halmashauri kuweza kuangalia namna ya kutengeneza barabara ya kutoka Fundi mpaka Seela Sokoni kwani barabara hiyo inachangia sana wanafunzi kuteseka hasa wakati wa mvua nyingi.
"Tunaipenda sana sekta ya elimu na shule zetu ya Seela lakini kwa kweli watoto wanateseka sana wakati wa mvua na hii inawafanya hata wengine kuwaza kuairisha shule kwa kuwa barabara ni mbovu"aliongeza Kuriye
Mwisho


No comments:
Post a Comment