Tanzania na Singapore zimefungua ukurasa mpya wa ushirikiano baada ya kusaini mikataba mitano na hati za makubaliano katika sekta mbalimbali.
Ziara ya siku tatu ya Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam, kwa mwaliko wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imeweka msingi wa kuimarisha diplomasia ya uchumi, biashara na uwekezaji.
Mikataba iliyosainiwa inahusu kuondoa kodi mara mbili, uendelezaji wa ujuzi, biashara za kaboni, mashauriano ya kidiplomasia na uwezeshaji wa biashara.
Rais Samia ameikaribisha Singapore kufungua ubalozi nchini na kusisitiza uwezeshaji wa vijana katika uchumi wa kidigitali.
Kwa upande wake, Rais Shanmugaratnam ameahidi kushirikiana katika kilimo, afya (kupambana na selimundu), na kufungua fursa kupitia soko huru la Afrika.
Ziara hii ya kihistoria inafanyika wakati Tanzania na Singapore zinaadhimisha miaka 45 ya uhusiano wa kidiplomasia.
Aidha, ushirikiano katika kilimo unatarajiwa kuongeza uzalishaji na kuimarisha usalama wa chakula, huku makubaliano ya biashara za kaboni yakionyesha dhamira ya pande zote mbili katika kulinda mazingira na kutekeleza mkataba wa Paris.
![]() |

.jpg)
No comments:
Post a Comment