Mkuu wa Wilaya Arumeru Afanya ziara shule za Enyuata na kiranyi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 9 June 2026

Mkuu wa Wilaya Arumeru Afanya ziara shule za Enyuata na kiranyi

 




Na Mwandishi wetu,Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Mwinyi A. Mwinyi amefanya ziara katika Shule za msingi Enyuata pamoja na Kiranyi katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha. 


Akiwa katika shule hizo, ambazo zipo eneo moja, amekagua miundombinu ya majengo, maji, umeme pamoja na mazingira kwa ujumla. 


Vilevile Mwinyi ametembelea eneo karibu na shule hizo ambalo halmashauri kushirikiana na Wananchi inatarajia kujenga kivuko katika eneo la mto chenye thamani ya shilingi milioni 53 ambapo tayari halmashauri imeshatenga kiasi cha shilingi milioni 40 kwaajili ya kazi hiyo.


Kwa nyakati tofauti wakizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Baraka Mesiaki pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, wamemhakikishia mkuu wa wilaya huyo kwamba muda si mrefu ujenzi wa kivuko hicho utaanza kwa kuwa bajeti yake imeshatengwa.


Akihitimisha ziara yake hiyo, pamoja na mambo mengine Mhe. Mwinyi amesisitiza suala la usafi pamoja na ulinzi wa miundombinu na wanafunzi katika shule hizo, ikiwa ni agizo kwa shule zote katika Wilaya ya Arumeru


"Kuanzia leo nitakuwa mlezi wa shule hizi mbili na nitoe agizo kwa shule zote zilizoko wilaya ya Arumeru kuhakikisha mazingira ya shule ni masafi wakati wote, ili kuwafanya Wanafunzi wafurahie masomo yao" amesema.


Ziara hiyo ina lengo la kuhakikisha mazingira ya kufundishia na kujifunza yanakuwa rafiki kwa walimu pamoja na wanafunzi ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani ya ndani na ya kitaifa.

No comments: