Rais Samia ataka mageuzi ya kiuchumi yaende sambamba na maisha ya wananchi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 12 June 2026

Rais Samia ataka mageuzi ya kiuchumi yaende sambamba na maisha ya wananchi

 



Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mageuzi yanayofanyika kwenye sekta ya fedha yanapaswa kuakisi maisha halisi ya wananchi, si kubaki katika takwimu.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Juni 12, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Ameeleza kuwa mageuzi yanayoyazungumza ni muhimu lakini kama hayatabadili maisha ya wananchi yatasalia kuwa takwimu katika ripoti.

“Takwimu zitasema kama tunvyoona upande kwingine, uchumi unapanda, GDP ni kubwa, uchumi wa nchi ni mkubwa lakini ukifika kwa watu hali za watu siyo nzuri,” ameeleza Dkt Samia na kuongeza kuwa;

“Msiposimamia vema, mabadiliko hayo yatabaki kuwa takwimu na ni vema kutafsiri ukuaji wa uchumi ili uende ukakue mpaka kwa mtu wa kawaida kule chini,” amesema.

Amefafanua kuwa mafanikio katika mifumo wa fedha hayana budi kwenda na mafanikio ya mwananchi mmoja. 

Dkt Samia kipimo kisibaki kuwa ni wananchi wangapi wamefikiwa   na huduma ya fedha, bali kiwe ni kwa kiasi gani huduma za fedha zinakuza mitaji na biashara ndogondogo na kuweza kuchangia kuwafanya wale wa biashara ndogondogo kuchangia katika uchumi wa nchi.

Katika hatua nyingine, Dkt Samia amezitaka taasisi za fedha nchini kuwa wabunifu katika kutafuta njia zitakazowawezesha kutoa mikopo kwa wananchi bila kuhitaji dhamana zilizozoeleka kama nyumba, gari au kiwanja, bali watumie uaminifu wao katika bishara wanazozifanya.

No comments: