RAIS SAMIA AWASILI MOSCOW KWA ZIARA YA KIKAZI NCHINI URUSI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 3 June 2026

RAIS SAMIA AWASILI MOSCOW KWA ZIARA YA KIKAZI NCHINI URUSI





Na Beda Msimbe, TBN, Moscow


maipacarusha20@gmail.com 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, uliopo Jijini Moscow kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa, nchini Urusi


Katika ziara hii ya kihistoria ikifanywa kwa mara ya pili katika historia ya uhusiano wa Tanzania na Urusi, ya kwanza ilikuwa ni miaka ya 1960 iliyofanywa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Samia anaendeleza kampeni kubwa ya kuhakikisha Tanzania inanufaika pia kiuchumi na uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali


 Kwa mujibu wa shughuli atakazofanya Rais Samia akiwa hapa nchini kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na kihistoria baina ya Tanzania na Urusi,Rais amekuja kuiweka Tanzania katika ramani ya uwekezaji kwa ushiriki wake katika mkutano mkubwa wa uwekezaji jijini St Petersburg na pia kuona namna ya kutengeneza raslimali watu ambayo taifa inahitaji sana katika kufanikisha utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2050. 


Alipowasili nchini hapa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, Jijini Moscow  majira ya saa mbili na dakika 25 usiku , japo jua bado lilikuwa linawaka,  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokea heshima ya wimbo wa Taifa pamoja na gwaride.


Rais Samia alipokewa uwanjani na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi Mhe. Maxim Reshetnikov. 


Kwa mujibu wa ratiba leo asubuhi ataanza na kuweka shada ka maua kwa kaburila askari asiyejulikana kabla ya kwenda Ikuku ya Kremlin kwa mazungumzo na Rais Vladmir Putin.


mwisho

No comments: