TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA UBELGIJI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 2 June 2026

TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA UBELGIJI






Na Mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com 


Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, CPA Mussa N. K. Juma akiongoza ujumbe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na TANAPA kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji.


Ujumbe huo ulipokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Ndg. Alphonce Mayalla, na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuhusu fursa za ushirikiano katika kuendeleza Uhifadhi, Utalii na Uwekezaji katika Hifadhi za Taifa Tanzania.


Miongoni mwa washiriki wa mazungumzo hayo walikuwa Katibu wa Diaspora wa Ubelgiji na Luxemburg, Ndg. Nahum Kisoky, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Gazeti la Diplomatic World, Bi. Barbara Dietrich.


Mazungumzo hayo ni katika juhudi za kuendeleza uhifadhi, utalii na uwekezaji katika maeneo ya Hifadhi za Taifa Tanzania.


#ESQR2026 #Brussels #TANAPA #DestinationTanzania

#TanzaniaParks #TanzaniaUnforgettable

No comments: