TTCL, Posta yaanza kupata faida - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 30 June 2026

TTCL, Posta yaanza kupata faida

 


Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Shirika la Posta, yameanza kuzalisha faida ndani ya Serikali, baada ya kipindi kirefu cha hasara.


Amesema mashirika hayo ni baadhi ya yale ambayo yalikabiliwa na changamoto za kifedha, mitaji na utegemezi mkubwa wa ruzuku na kwa sasa yameanza kurejea katika hali ya kujiendesha kwa tija.


Mchechu ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Jumanne Juni 30, 2026 alipozungumza katika Siku ya Gawio ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ni mgeni rasmi.


Amesema TTCL imezalisha faida ya Sh22.9 bilioni mwaka huu, kutoka hasa ya Sh18 bilioni iliyoipata katika mwaka wa fedha uliopita. Kwa faida hiyo, shirika hilo limetoa gawio la Sh1.6 bilioni.


Kwa upande wa Shirika la Posta, amesema limepata faida ya Sh2.8 bilioni na limetoa sehemu ndogo ya gawio.

No comments: