UHASIBU ARUSHA WAJA NA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTALII - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 17 June 2026

UHASIBU ARUSHA WAJA NA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTALII

 




Na Mwandishi wetu..Aruaha


maipacarusha20@gmail.com 


Chuo cha uhasibu Arusha  kinatarajia kukutanisha wadau mbali mbali wa sekta utalii kutoka  ndani na nje ya nchi katika kongamano la utalii  la  kimataifa litakalofanyika September  24  mwaka huu   ikiwa ni fursa ya  kutangaza nchi kwenye sekta ya utalii.



Akizungumza katika ufunguzi  wa  maandalizi  ya kongamano  hilo, uliofanyika katika  chuo cha Uhasibu Arusha naibu  mkuu wa chuo   upande wa taaluma ,tafiti na ushauri  wa kitaallam chuo cha uhasibu Arusha  dkt Grace Temba  alisema kuwa wameanza maandalizi mapema kwani ni la muhimu sana kwa wadau wote wa utalii


Alisema kuwa wanatarajia kongamano  la mwaka ambalo ni la nne kufanyika chuoni hapo  linakutanisha wadau mbali mbali wa sekta ya utalii kutoka hapa nchini na nje ya Tanzania pamoja na  kimataifa na kwamba ni la muhimu sana kwa taasisi hiyo wadau pamoja na serikali. 


" katika kongamano letu hili tunatarajia kukutanisha  watunga sera wa taaaisi na watafiti wa  sekta ya utalii pamoja na wadau  ambao watasaidia kutoa maboresho ya sekta ya utalii  ambayo yatanufaisha pande zote lakini na chuo  chetu kitatoa tafiti zake"aliongeza 


Naye kaimu mkuu wa kitivo jinsia na sayansi ya jamii  Lorna Mwijarubi alieleza kuwa mwitikio wa konhamano hilo ni mkubwa kwani wamepata mafanikio makubwa ikiwemo wadau kuwapatia wanafunzi wa chuo hicho naffasi ya mafunzo ya vitendo ambayo yamewawezesha kujifunza mambo ya utalii na ukarimu.


 Alisema katika kongamano hilo  wanatarajia  kupata ubunifu na tafiti mbali mbali ambazo zitawezesha kuongeza uzoefu kwenye utalii.




Joaiven Karama ni Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo cha uhasibu Arusha  alisema kongamano hilo  ambalo ni la mara ya nne limewasaidia kutambulisha kozi ya utalii  na ukarimu  inayofundishwa chuoni hapo pamoja na kupata uwanda mkubwa wa kukutana na wadau  wa utalii ambao wamewaongezea uzoefu.

No comments: