Rais Samia Suluhu Hassan, amesema penye siasa za chuki na mivutano, maendeleo hutoweka, huku panapokuwa na siasa za staha na maridhiano, maendeleo hupata nafasi na kuchanua.
Amesema hatua iliyofikiwa Zanzibar, ni makubaliano ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuanza mazungumzo ya mustakabali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais Samia ameyasema hayo visiwani Zanzibar leo, Alhamisi Julai 9, 2026 alipohutubia wakati wa hafla ya utiaji saini Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa Zanzibar.
Ametoa wito wa kuheshimiwa kwa makubaliano hayo na kuendeleza mazungumzo kwa uwazi na kuaminiana, huku misingi ya umoja, amani, usalama na utulivu wa Taifa ukizingatiwa.
Ameeleza hekima iliyoonyeshwa ikalindwe kwa matendo mema ya kesho na imani iliyojengwa kwa muda mrefu isiangushwe kwa maneno au mienendo isiyo na tija.

No comments:
Post a Comment