Tanroad Arusha Kuing'arisha Monduli kwa taa za barabarani - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 6 July 2026

Tanroad Arusha Kuing'arisha Monduli kwa taa za barabarani

 

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha Mhandisi  Reginald Masawe

Na Mwandishi wetu, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com 



 Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Mkoa wa Arusha umesema utaweka taa 40 za nishati ya jua katika Wilaya ya Monduli katika mwaka wa fedha 2026/2027 ili kupunguza ajali na kuwasaidia wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao usiku.


Hayo yamesemwa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Masawe, katika kikao na madiwani pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Monduli. Kikao hicho kilifanyika kufuatia maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha.


“Kwa mwaka wa fedha huu tumejipanga kuweka taa 40 za nishati ya jua wilayani Monduli. Hii itasaidia sana wafanyabiashara na kupunguza ajali usiku,” amesema Mhandisi Masawe.


Ameongeza kuwa TANROADS itaangalia uwezekano wa kuweka taa maeneo mengine ikiwemo Meserani, pamoja na kufanya tathmini ya vyanzo vya mafuriko ili kuweka mikakati ya kupunguza athari zake.


*Maombi ya madiwani*  

Akizungumza katika kikao hicho, mheshimiwa Diwani Kimai, wa Kata ya Sepeko ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ameshauri Serikali iharakishe mchakato wa `kupanda msitu wa Lendikinya` na kulinda sehemu iliyobaki kwa gharama kubwa.


Pia ameiomba TANROADS kuiwekea `stendi taa` Sekondari ya Nanja, pamoja na Soko la Nanja, kwani wakati mwingine wanawake wanateseka sana hasa majira ya usiku


Mbali na hayo pia  alisema eneo hilo halina miundombinu hiyo ambayo ni muhimu kwa usalama wa wanafunzi na wafanyabiashara.


*MWISHO*

No comments: