Mwandishi wetu, ARUSHA
maipacarusha20@gmail.com
Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na Tanzania Roads Association (TARA) na Tanzania Transportation Technology Transfer Centre (TanT² Centre), kwa ushirikiano na taasisi mbalimbali za ndani na kimataifa wamefanya mafunzo ya wataalamu wa ujenzi wa barabara ili kuimarisha miradi ya miundombinu kukidhi viwango vya kimataifa.
Mafunzo hayo yameanza Agosti 10 hadi 15, 2026 jijini Arusha na kuwashirikisha wataalamu toka nchi za Tanzania, zimbabwe, Ethiopia na wengine wakishiriki kwa njia ya mtandao toka nchini Afrika ya kusini.
Katika mada zilizowasilishwa,na mhandisi, Deogratius mugishagwe, washiriki wamejifunza misingi ya ujenzi wa barabara ikiwemo hatua za ujenzi, usimamizi wa kazi za eneo la mradi, tabaka za lami, matumizi ya vifaa vinavyokidhi viwango, vipimo vya udhibiti wa ubora, mifumo ya mifereji ya maji, pamoja na wajibu wa msimamizi wa mradi katika kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ubora.
Aidha, mafunzo hayo yameangazia kanuni za usanifu wa barabara, uainishaji wa barabara, usanifu wa madaraja na mifumo ya kupitisha maji, pamoja na viwango vya ujenzi wa barabara vinavyotumika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza uwezo wa wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa barabara na wadau wengine wa sekta hiyo, ili kuboresha ubora wa miundombinu na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya barabara nchini.
Washiriki wa mafunzo hayo ni wahandisi watanzania, zimbabwe, Ethiopia na wengine wakishiriki kwa njia ya mtandao nchini Afrika ya kusini na wanachama wa Africa Mashariki.
Mafunzo haya yatamalizika kwa ziara ya kutembelea miradi ya tarura katika mradi ya ujenzi wa miundo mbinu ya Afcon.



No comments:
Post a Comment