COPRA YAHAMASISHA MATUMIZI YA MIFUMO YA KIDIGITALI KUBORESHA BIASHARA YA MAZAO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 6 August 2026

COPRA YAHAMASISHA MATUMIZI YA MIFUMO YA KIDIGITALI KUBORESHA BIASHARA YA MAZAO






 Lilian Kasenene, Morogoro



maipacarusha20@gmail.com


MAMLAKA ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania (COPRA) imewataka wakulima na wafanyabiashara wa mazao nchini kutumia mifumo ya kidigitali katika kurahisisha biashara na kuongeza ushindani wa mazao katika masoko ya ndani na nje ya nchi.


Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa COPRA, Mary Majule, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro.


Majule alisema banda la COPRA linaendelea kutoa elimu kwa wakulima na wadau mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo, zikiwemo usajili wa wafanyabiashara, utoaji wa leseni na vibali, pamoja na taratibu za biashara ya mazao.


"Katika banda letu tunatoa elimu kwa wakulima na wadau mbalimbali kuhusu mifumo yetu ya kidigitali na namna wanavyoweza kuitumia kupata huduma mbalimbali kwa urahisi na kwa wakati," alisema.


Alisema matumizi ya mifumo hiyo yanalenga kuhakikisha biashara ya mazao inafanyika kwa uwazi, haki na ushindani, sambamba na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.


Kwa mujibu wa Majule, COPRA imejikita katika kuimarisha uzalishaji na biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko, kuendeleza mifumo bunifu ya kidigitali na takwimu, kuimarisha masoko yenye ushindani, kuboresha utendaji wa taasisi na kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wa sekta hiyo.


Alifafanua kuwa mamlaka hiyo inatumia mfumo wa kisasa wa **COPRA MIS** unaowezesha utoaji wa leseni na vibali, usimamizi wa mikataba ya kilimo kati ya wakulima na wanunuzi au wawekezaji, pamoja na uhakiki wa ubora wa mazao kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa.


Mbali na hilo, alisema mfumo huo unasaidia kufuatilia mazao katika mnyororo mzima wa thamani kuanzia shambani hadi sokoni, hatua inayochangia kuongeza uwazi, ufanisi na tija katika biashara ya mazao nchini.


....

No comments: