Kizimkazi Festival yabeba matumaini ya wananchi katika miradi, Wananchi wapata matumaini miradi itakayozinduliwa Kizimkazi Festival - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 7 August 2026

Kizimkazi Festival yabeba matumaini ya wananchi katika miradi, Wananchi wapata matumaini miradi itakayozinduliwa Kizimkazi Festival

 



Mwandishi Wetu maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Wakazi wa Kizimkazi visiwani Zanzibar, wamesema Tamasha la Kizimkazi litakuwa zaidi ya burudani, kwa kuwa litaambatana na uzinduzi wa miradi ya maendeleo itakayowanufaisha kiuchumi.


Miradi hiyo itakayozinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi ni Jengo la Maendeleo la Shehiya Kibuteni, Barabara ya Kichakachindi–Mtondooni (KM 3.1), Hoteli ya Cave, Tenki la maji la lita milioni 1.5 na mradi wa nyumba za Bopar.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema tamasha hilo limekuwa likiongeza ajira za muda kwa vijana, kukuza biashara na kuboresha huduma za kijamii.


Wamesema uzinduzi wa tenki la maji utasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji na kuboresha maisha ya wananchi.


Tamasha hilo lenye kaulimbiu ya 'Kizimkazi Kumenoga: Shangwe na Fursa' linatarajiwa kufanyika Agosti 12 hadi 14, mwaka huu.

No comments: