Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi, amemwandikia Rais Samia Suluhu Hassan, barua ya kujiuzulu wadhifa huo, miezi michache baada ya kutoa kauli mbalimbali zenye utata.
Kabla ya taarifa hiyo, Dk Nchimbi kwa nyakati tofauti amekuwa akiibua kauli zinazoleta utata, ikiwemo ile aliyowataka Watanzania wapambane kuipata Katiba Mpya, ilhali ajenda hiyo tayari ilishawekewa utaratibu ndani ya chama chake cha CCM na hata kuwa katika Ilani ya chama hicho.
Kauli hiyo iliibua sintofahamu hata ndani ya CCM. Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Fadhili Maganya, aliijibu kwa kuhoji, anayewashinikiza Watanzania wapambane kupata Katiba Mpya, anataka wapambane na nani?
Sambamba na kauli ya Maganya, Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi, Mohamed Simai Said, aliwahi kusema ndani ya Serikali kuna kiongozi msaliti akimwita ‘Yuda’ kwa kile alichosisitiza, anakinzana na mwelekeo na dhamira ya Serikali.
Mienendo hiyo, ilimwibua Mwanasiasa mkongwe, John Shibuda ambaye Agosti 23, 2026 alizungumza na vyombo vya habari, akimsihi Dk Nchimbi ajiuzulu kutokana na mwenendo wake unaokwenda kinyume na mwelekeo wa Serikali
Dk Nchimbi ametoa taarifa ya kuandika barua ya kujiuzulu na kusambaza katika kurasa za mitandao yake ya kijamii leo, Agosti 25, 2026.
Katika barua yake, ameandika atajiuzulu wadhifa huo kuanzia Septemba 4, 2026 akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi kwa kipindi alichoongoza.Hata hivyo hadi sasa hakuna tamko rasmi la Serikali au la Dk Nchimbi kujitokeza hadharani kuhusiana na kujiuzuru kwake.

No comments:
Post a Comment